Music

Mbosso – Haijakaa Sawa (Mp3 Download, Lyrics)

Haijakaa Sawa by Mbosso (Mp3 Download, Lyrics)

Download Haijakaa Sawa Mp3 by Mbosso

Download Mp3

Video: Haijakaa Sawa by Mbosso

Haijakaa Sawa Lyrics by Mbosso

Sasa unanuna nini?
Au unadhani hata mimi napenda
Nishazichoka na mimi
Mboga za majani kila siku mlenda

Siko juu siko chini
Niko nusu sadoo
Sio wa kumi si sabini
Ngoma ngumu bado
Kama ibada naswali sana
Usiku wa manane
Tena nafunga na Suna
Mambo bado bado mwana wane
Naona yanazidi kuguma
Nikirudi na hasira hasira (nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (niombee)
Nikirudi na hasira hasira (nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (niombee)

Halijakaa sawa
Nivumilie ipo siku tutapata
Halijakaa sawa
Shida na dhiki zitakwisha baby
Halijakaa sawa
Kuchana kope make up utapaka
Halijakaa sawa
Tutabadili mboga kuku kwa manyama
Chochea kuni kipenzi changu
Asubuhi tumbo likikuming’inya
Pokea kidogo changu

Tunywe chai na mkate wa kumimina
Akili ikichoka riziki nikikosa
Najua kwako nitajiliwaza
Kama makosa nivute chumbani
Kununa nuna unajilemaza
Ustahimilivu mnao wachache mno
Jua shida rafiki wa mbivu

Baada ya dhiki mavuno
Kila jema lina maumivu
Na kwenye waliopo tumo
Yarabi salama tupe tulivu
Penzi lisifike kikomo
Iyee eeh eeh
Nikirudi na hasira hasira (nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (niombee)
Nikirudi na hasira hasira (nizoee)
Mambo magumu bado bila bila (niombee)

Halijakaa sawa
Nivumilie ipo siku tutapata
Halijakaa sawa
Shida na dhiki zitakwisha baby
Halijakaa sawa
Kuchana kope make up utapaka
Halijakaa sawa
Tutabadili mboga kuku kwa manyama

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *